MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp anadaiwa kuwa tayari kumuwania winga wa Anderlecht Frank Acheampong katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Klopp amekuwa akituma watu wake wamfuatilie nyota huyo wa kimataifa wa Ghana mara kadhaa na sasa anafikiria kumchukua kabisa Januari. Ingawa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 huwa anacheza kama winga wa upande wa kushoto lakini pia anaweza kucheza kama beki wa kushoto, idara ambayo Klopp anataka kuiboresha zaidi. Acheompong ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Ubelgiji miaka mitatu iliyopita, anatarajiwa kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika mwezi ujao hatua ambao inaweza kuyumbisha usajili wake huo.
No comments:
Post a Comment