SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, imelitaka Shirikisho la Soka la nchini hiyo kusimamisha mechi za ligi kuanzia leo mpaka hapo itakapotolewa taarifa zaidi. Hatua hiyo imekuja kufuatia hofu ya vurugu pindi rais Joseph Kabila atakapomaliza muda wake wa kuwepo madarakani wiki ijayo. Katibu Mkuu wa wizara ya michezo ya nchi hiyo, Barthelemy Okito amesema wanahofu jinsi hali ilivyo hivi sasa inaweza kuhamia viwanjani na kuhatarisha maisha ya watu. Kikatiba muda wa rais Kabila kukaa madarakani unamalizika Desemba 19 mwaka huu lakini mwenyewe ameshasema kuwa ataendelea kuwepo madarakani mpaka Aprili mwaka 2018 wakati serikali itakapokuwa imejipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine baada ya ule wa mwaka huu kuvurugika.
No comments:
Post a Comment