Wednesday, December 7, 2016

MMILIKI WA NDEGE ILIYOUA WACHEZAJI WA CHAPECOENSE AKAMATWA.

MAMLAKA nchini Bolivia imemkamata kiongozi wa Shirika wa Ndege iliyohusika katika ajali iliyoua watu 71 wengi wao wakiwa wachezaji wa timu ya soka ya Chapecoense nchini Brazil. Gustavo Vargas ambaye ni generali mstaafu wa jeshi alikamatwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaondelea kung’amua chanzo cha ajali hiyo. Ndege hiyo ya kampuni ya LaMia ilikuwa imebeba wachezaji wa timu hiyo ikiwapeleka nchini Colombia wakati ilipoishiwa na mafuta. Maofisa wa Bolivia wamesema rubani wa ndege hiyo alionywa kuhusiana na tatizo hilo kabla ya haijaondoka. Chapecoense walikuwa wakisafiri kwenda katika mji wa Medellin kucheza mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Copa Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional.

No comments:

Post a Comment