CHAMA cha Vilabu Ulaya-ECA kimeponda mipango ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutaka kuongeza timu kufikia 48 katika Kombe la Dunia na kulituhumu shirikisho hilo kupuuza maadili ya soka kwa ajili ya fedha na siasa. Wakati akigombea, rais wa FIFA Gianni Infantino moja ya mipango yake ilikuwa ni pamoja na pendekezo la kuongeza timu katika fainali hizo kutoka 32 za hivi sasa mpaka 40. Mapema mwezi Octoba, Infantino alidokeza fainali hizo zinaweza kuongezeka zaidi kwa kuongeza nchi washiriki kufikia hadi 48. Hata hivyo, ECA wamepinga vikali hatua hiyo ya kuongeza ukubwa wa michuano hiyo kwani kwa kufanya hivyo inamaanisha kutuakuwa na mechi nyingi zaidi kwa wachezaji kwa mwaka. Mwenyekiti wa ECA, Karl-Heinz Rummenigge amesema kwa maslahi ya mashabiki na wachezaji FIFA haipaswi kuongeza ukubwa wa michuano hiyo.

No comments:
Post a Comment