Thursday, January 5, 2017
RODRIGUEZ ADAI HAENDI POPOTE.
KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Colombia, James Rodriguez amemaliza uvumi ulioenea kuhusu kuondoka Real Madrid kwa kithibitisha kuwa ataendelea kubakia katika klabu hiyo na kupigania nafasi yake.
Tetesi hizo za kuondoka kwa nyota huyo zilizivuta klabu za Chelsea, Paris Saint-Germain na Manchester United kuanza kumnyemelea.
Mwezi uliopita Rodriguez aliongeza uvumi huo baada ya kusai kuwa amepata ofa ya kuondoka na hakuthibitisha kama ataendelea kubakia Santiago Bernabeu.
Lakini baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sevilla jana katika mchezo wa Kombe la Mfalme, nyota huyo sasa ameamua kubakia klabu hapo baada ya kufanya mazungumzo na meneja wake Zinedine Zidane.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment