Wednesday, May 2, 2012
SIJASHANGAZWA NA UTEUZI WANGU - hODGSON.
KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema kuwa hakushangazwa na uteuzi wake wa kukalia kiti hicho ambacho kiliachwa na Fabio Capello pamoja na kwamba wengi walitabiri Harry Redknapp angechukua nafasi hiyo. Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA David Bernstein alifafanua kuwa kamati teule ambayo ilikuwa na watu wanne ambao walikuwa wanataka nafasi hiyo tayari ilikuwa imeshafanya maamuzi ya kumteua Hodgson ambaye alikuwa kocha wa West Brom mwezi mmoja uliopita. Hodgson ambaye ana umri wa miaka 64 alikabidhiwa mkataba wa miaka minne wa kuinoa timu hiyo jana ambapo alisisitiza kuwa rekodi yake nzuri na uzoefu alionao ndio umechangia kwa kiasi kikubwa kupata kibarua hicho. Kocha huyo amekiri kuwa bado ana changamoto kubwa ya kujaribu kurejesha imani ya wachezaji kwake wakiwemo wale ambao walikuwa wakimpa nafasi kubwa Redknapp kuchukua nafasi hiyo baada ya Capello kujiuzulu.
Tuesday, May 1, 2012
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.
NGORONGORO HEROES KWENDA SUDAN MEI 2
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) inatarajia kuondoka kesho (Mei 2 mwaka huu) kwenda Sudan kwa ajili ya mechi dhidi ya Sudan itakayochezwa Mei 5 mwaka huu. Msafara wa Ngorongoro Heroes utakaokuwa na watu 28 ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Kambi utaondoka saa 8.45 mchana kwa ndege ya Kenya Airways. Ngorongoro Heroes itaagwa rasmi kwa kukabidhiwa Bendera ya Taifa kesho (Mei 2 mwaka huu) saa 5 kamili asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Wengine katika msafara huo ni wachezaji na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Kim Poulsen. Mechi hiyo ya marudiano namba 16 itachezwa kwenye Uwanja wa Khartoum kuanzia saa 2 kamili usiku kwa saa za Sudan. Iwapo Ngorongoro Heroes ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 3-1 itafanikiwa kuitoa Sudan itacheza na Nigeria ambayo yenyewe imefuzu moja kwa moja kucheza raundi ya pili ya michuano hiyo. Mechi ya kwanza itachezwa Julai 28 jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itafanyika Nigeria kati ya Agosti 10, 11 na 12 mwaka huu. Fainali za U20 kwa Afrika zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria.
MECHI KUCHANGIA TWIGA STARS SASA MEI 6
Mechi maalumu ya hisani kwa ajili ya kuchangia timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars), kati ya timu hiyo na wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie itachezwa sasa itachezwa Mei 6 mwaka huu badala ya Mei 4 mwaka huu. Kwa mujibu wa kampuni ya Edge Entertainment iliyoandaa mechi hiyo, imesogezwa mbele kwa siku mbili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kujitokeza kuchangia Twiga Stars. Awali ilikuwa ichezwe Ijumaa ambayo ni siku ya kazi, hivyo imesogezwa hadi Jumapili ambayo ni siku ya mapumziko. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni ambapo viingilio kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu ni sh. 2,000, VIP C na B itakuwa sh. 5,000 wakati VIP A ni sh. 10,000. Twiga Stars ambayo kwa sasa haina mdhamini na kambini katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani kujiandaa kwa mechi ya mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia. Timu hizo zitapambana Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa na kurudiana Juni 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshindi atashiriki fainali za AWC zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
RUFANI YA AFRICAN LYON KUJADILIWA MEI 2
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana Mei 2 mwaka huu kujadili rufani iliyowasilishwa mbele yake na klabu ya African Lyon. Klabu hiyo ya Ligi Kuu inailalamikia TFF ikipinga uamuzi uliofanywa na Kamati yake ya Ligi juu ya kuvunjika kwa pambano la ligi hiyo kati ya Azam na Mtibwa Sugar lililochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Katika rufani yake, Lyon imedai uamuzi uliofanywa na Kamati ya Ligi ya TFF haikuwa sahihi, kwani haukuzingatia kanuni za ligi hiyo kuhusu timu inayogomea mchezo. Kamati hiyo chini ya Kamishna Mstaafu wa Polisi, Alfred Tibaigana inatarajia kufanya kikao chake kuanzia 8 mchana.
PONGEZI KWA TIMU YA SIMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa timu ya Simba kwa ushindi wa mabao 3-0 ambao iliupata juzi (Aprili 29 mwaka huu) dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan katika mechi ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa Dar es Salaam. Ushindi huo umetokana na ushirikiano uliopo kuanzia kwa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama wa klabu hiyo na Watanzania kwa ujumla. Ni imani ya TFF kuwa Simba haijabweteka kwa ushindi huo na badala yake sasa inajipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa nchini Sudan ili kuondoa Al Ahly Shandy kwenye michuano hiyo na kusonga mbele. TFF kama kawaida itaendelea kutoa ushirikiano kwa Simba ili kuhakikisha inafika mbali kwenye mashindano hayo, na ikiwezekana kuandikika historia ya kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kutwaa Kombe la Shirikisho.
PAZIA LIGI KUU VPL KUFUNGWA MEI 5
Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2011/2012 kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itafikia tamati Mei 5 mwaka huu kwa bingwa kujulikana ambapo timu zote 14 siku hiyo zitakuwa uwanjani. Klabu kongwe za mpira wa miguu nchini Simba na Yanga zitakutanisha timu zao katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Nayo Oljoro JKT itakuwa mwenyeji wa Polisi Dodoma katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha na Ruvu Shooting itacheza na Villa Squad katika Mabatini, Mlandizi. Mechi nyingine zitakuwa kati ya Coastal Union na Toto African itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, African Lyon na JKT Ruvu (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Azam na Kagera Sugar (Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam) na Moro United na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro). Kwa mujibu wa kanuni namba 4(2)(c) ya Ligi Kuu ya Vodacom, timu tatu za mwisho katika msimamo wa ligi zitashuka daraja. Tayari Moro United na Polisi Dodoma zimeshashuka, iliyobaki itajulikana baada ya mechi za Jumamosi ambazo zote zitaanza saa 10 kamili jioni.
MIKOA SITA YAOMBA UENYEJI LIGI YA TAIFA
Mikoa sita imeshaomba kuwa wenyeji wa Ligi ya Taifa itakayochezwa katika vituo vitatu tofauti. Ligi hiyo inayoshirikisha mabingwa wa mikoa inatarajia kuanza baadaye mwezi huu. Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana wakati wowote kupitia maombi hayo kabla ya kufanya uamuzi wa vituo na tarehe ya kuanza ligi hiyo. Mikoa iliyoomba vituo ni Dar es Salaam, Kigoma, Lindi, Mara, Shinyanga na Singida.

ROCK STAR GALLAGHER AVAMIA POST-MATCH PRESS CONFERENCE BAADA YA KUPAGAWA NA USHINDI WA CITY.
![]() |
| Gallagher akiwa na Maradona mara baada ya mchezo wa Manchester City na Manchester United. |
FERGUSON AMTUHUMU MANCINI KUWABUGUDHI WAAMUZI.
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amemtuhumu kocha Manchester City Roberto Mancini kwa kuwasumbua waamuzi baada ya makocha hao kugombana wakati wa mchezo baina ya timu hizo ulichezwa jana. Ferguson na Mancini ilibidi watenganishwe baada ya kushindwa kuzuia jazba zao kwa kunyoosheana vidole dakika ya ya 76 ya mchezo huo ambao City walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Ferguson alinyanyuka kutoka alipokuwa amekaa na kuanza kulalamika mchezo mbaya aliochezewa mshambuliaji wa timu yake Danny Welbeck na beki wa City Nigel De Jong. Kocha huyo ambaye ana miaka 70 alimtuhumu Mancini kuwabugudhi waamuzi katika kipindi chote cha msimu huu lakini akahoji kwanini kocha huyo hajalalamikia mchezo huo.
KOCHA WA MALI AREJEA BAADA YA MACHAFUKO KUTULIA.
KOCHA wa timu ya taifa ya Mali, Alain Giresse amerejea baada ya kuondoka na familia yake kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini humo. Giresse mwenye umri wa miaka 59 anatarajiwa kusaini mkataba mpya baadae wiki hii na Shirikisho la Soka la nchi hiyo kufuatia mkataba wake wa awali ambao ulikuwa wa miaka miwili kuisha Februari mwaka huu. Kocha huyo alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo na kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikiwa ni rekodi ya juu kabisa kuwekwa na nchi hiyo katika miaka 40 iliyopita. Taarifa zilizozagaa jijini Bamako zinasema kwamba kocha huyo ambaye ni raia wa Ufaransa atapewa mkataba wa mwaka mmoja ambapo mkataba huo unaweza kuongezwa kama timu hiyo ikifanikiwa kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014. Mali imepangwa katika kundi H ikiwa na timu za Algeria, Benin, na Rwanda ambapo June 6 mwaka huu inatarajiwa kucheza na Benin katika mzunguko wa pili kabla ya kuikaribisha Algeria jijini Bamako wiki moja baadae.
REDKNAPP AMKUBALI HODGSON KUINOA UINGEREZA.
MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Harry Redknapp amesema kuwa haoni tatizo mpinzani wake Roy Hodgson kupewa kibarua cha kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza. Redknapp amekuwa akitajwa kukinoa kikosi hicho toka aliyekuwa kocha wa timu hiyo Fabio Capello alipojiuzulu wadhifa huo Februari ambapo Chama cha Soka cha Uingereza-FA kimeamua kuanza mazungumzo ya awali na Hodgson ambaye ni kocha West Bromwich Albion. Hodgson ambaye ana miaka 64 amewahi kushinda mataji nane ya ligi katika nchi mbili tofauti akiwa anafundisha vilabu vitatu tofauti ambapo pia amewahi kuzifundisha timu za Switzerland, Finland na Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE. Kocha huyo alikutana na viongozi wa FA jana katika mkutano uliochukua muda wa saa nne uliofanyika katika Uwanja wa Wembley jijini London. Redknapp amesema kuwa kwasasa anafurahishwa na kibarua chake katika klabu ya Tottenham na anamtakia mafanikio Hodgson kama atapewa kibarua cha kionoa timu hiyo kwani anaamini anaiweza kazi hiyo kutokana na uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika soka ya kimataifa. FA inatarajiwa kumtangaza Hodgson kama kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo baadae leo mbele ya vyombo vya habari.
Subscribe to:
Posts (Atom)