Thursday, January 3, 2013
YANGA KUJIPIMA NGUVU NA ARMINIA BIELEFELD YA UJERUMANI HUKO UTURUKI.
Timu ya Young Africans Sports Club yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam nchini Tanzania siku ya jumamosi itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya kutoka nchini Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya. Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani ambayo pia imekuja kambi y amafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la pili nchini Ujerumani. Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo inawachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia. Unajua tun siku sita (5) tangu tufike hapa mjini Antalya Uturuki na tumeshafanya mazoezi kwa siku nne (4) hivo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu alisema 'Brandts' Arminia Bielefeld imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na timu ya Young Africans ambao ni mabingwa mara 23 katika ligi kuu ya Tanzania. Leo asubuhi Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa siku ya jumamosi mjini Antalya. Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.
MANCINI, BALOTELLI NUSURA WAZICHAPE MAZOEZINI.
Balotelli mwenye umri wa miaka 22 baadae alionyeshwa akitenganishwa na Mancini huku akiwa ameshikwa na ofisa mmoja wa timu hiyo ikiwa ni tukio la kushangaza wakati City ikijiandaa na mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Watford. Mancini alichukia kufuatia Balotelli kumchezea vibaya mchezaji mwenzake anayesadikiwa kuwa Scott Sinclair katika mazoezi hayo ambapo kwa mara nyingine tukio hilo linamuweka nyota huyo katika mlango wa kutokea. Tukio hilo limekuja ikiwa ni siku moja imepita toka mchezaji mwenzake wa zamani katika klabu ya Inter Milan, Zlatan Ibrahimovic kudai kuwa Balotelli ndio chaguo sahihi kwa City katika kutetea taji lao la Ligi Kuu nchini Uingereza.
BA ATIMKIA CHELSEA.
ALIYEKUWA mshambuliaji nyota wa klabu ya Newcastle United, Demba Ba amekamilisha usajili wake kwenda Chelsea huku kocha Alan Pardew akisisitiza kuwa nyota huyo ameondoka kwa Baraka zote za klabu. Ba mwenye umri wa miaka 27, mapema leo alikuwa kwenye mazungumzo na Chelsea kuhusiana na maslahi yake binafsi baada ya klabu hiyo kukubali kulipa kiasi cha paundi milioni 7.5 kwa Newcastle. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal aliachwa katika kikosi kilichopambana na Everton jana usiku na Pardew alifunguka kwa kusema mshambuliaji huyo wa zamani wa West Ham United ameshakubaliana maslahi binafsi na Chelsea. Ba alijiunga na Newcastle mwaka 2011 akitokea West Ham na amefunga mabao 29 katika michezo 54 ya ligi aliyocheza. Newcastle kwasasa inamfukuzia mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Olympique Marseille, Loic Remy ili kuziba pengo la Ba
KIPA NAMBA MOJA WA ZAMANI WA URUGUAY AFARIKI DUNIA.
Wednesday, January 2, 2013
VILANOVA AANZA KAZI RASMI.
MENEJA wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova amerejea mapema kuliko ilivyotegemewa na kuonekana mazoezini jana kwa mara ya kwanza toka alipofanyiwa upasuaji wa koo wiki mbili zilizopita. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 alihitaji upasuaji mwingine kufuatia upasuaji aliofanyiwa mara ya kwanza kuondoa uvimbe wa kansa katika koo lake Novemba 2011 na msaidizi wake Jordi Roura kuchukua nafasi yake wakati akijiuguza. Vilanova alitegemewa kurejea tena uwanjani katikati ya Januari lakini aliwatembelea wachezaji jana asubuhi na baadae kuwasimamia wachezaji mazoezini katika kipindi cha mchana. Wachezaji wengi katika kikosi hicho walikuwa hawapo kwasababu ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria huku nyota wengine wakiwa ndege zao zikiwa zimechelewa kufika wakati wakitoka katika mapumziko ya sikukuu za Noel na mwaka mpya.
MOURINHO APATA PIGO LINGINE.
MENEJA wa Real Madrid, Jose Mourinho amepata pigo lingine katika kikosi chake baada ya beki wake nyota Pepe kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kulia jana hivyo kuzidi kumuongezea tatizo katika safu yake ya ulinzi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao wa klabu hiyo Pepe alikuwa akijisikia maumivu katika mguu wake huo ambapo baada ya vipimo ilibidi afanyiwe upasuaji wa haraka jijini Porto, Ureno. Taarifa hiyo haikufafanua ni muda gani haswa Pepe ambaye ni raia wa Ureno atakaa nje akijiuguza lakini vyombo vya habari nchini Hispania vimeripoti kuwa atakuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja. Madrid imekuwa ikikabiliwa na matatizo katika safu yake ya ulinzi baada ya mabeki wake tegemeo kuwa majeruhi katika wiki za karibuni wakiwemo Fabio Coentrao na Marcelo. Kikosi cha Mourinho kwasasa kinashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 17 alama saba nyuma ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili na alama 16 nyuma ya mahasimu wao Barcelona ambao wanaongoza La Liga.
Subscribe to:
Posts (Atom)






