Sunday, February 3, 2013
Friday, February 1, 2013
EMIRATES KUENDELEA KUIDHAMINI PSG.
SHIRIKA la ndege la Emirates limefikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya wa udhani wa fulana za klabu ya Paris Saint-Germain-PSG inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Makamu wa rais wa Shirikisho hilo Boutros Boutros alithibitisha taarifa hizo mbele ya vyombo vya habari na kudai kuwa taratibu za kumalizia kupitia mikataba zinafanyika na mawakili wa pande zote mbili kabla ya kusaini baadae mwezi huu. Mwaka uliopita mmiliki wa klabu hiyo raia wa Qatar aliripotiwa kuwa katika mazungumzo na benki moja ya Qatar ambayo haikutajwa jina lake lakini Boutros amekana tetesi hizo na kudai klabu hiyo haikuzungumza na kampuni nyingine. Nembo ya Emirates imekuwa ikionekana katika jezi za PSg toka mwaka 2006 na mkataba wa sasa ambao unaishia mwaka 2014 una thamani ya dola milioni 5.5 kwa mwaka.
STERLING ASHITAKIWA KWA KUMSHAMBULIA MWANAMKE.
WINGA wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Liverpool, Raheem Sterling ameshitakiwa kwa kumshambulia mwanamke na kesi yake inatarajiwa kusikilizwa baadae mwezi huu. Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kuwa Sterling mwenye umri wa miaka 19 mzaliwa wa Jamaica aliletewa barua ya kuitwa mahakamani katika uwanja wa vijana jijini Liverpool jana. Polisi wamesema mwanamke mwenye umri wa miaka 27 ambaye alikuwa akijuana na mchezaji huyo alikuwa na majeraha wakati akiwakilisha tuhuma hizo huko Toxteth, Liverpool Nevemba 2 mwaka jana. Sterling ambaye aliwakilishwa na wakili wake Mick Hogan katika usikilizwaji wa shauri hilo alikataa tuhuma hizo za kushambualia.
FIFA PEKEE HAIWEZI KUPAMBANA NA VITENDO VYA RUSHWA KWENYE SOKA - BLATTER.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter amesema kuwa vita dhidi ya vitendo vya rushwa katika mchezo wa soka haviweza kupiganwa na wao pekee bali pia mashirikisho kutoka pande zote duniani inabidi watoe ushirikiano. Blatter anaamini kuwa wanachama 209 wa FIFA pamoja na mashirikisho ya mabara wanatakiwa kufuata mfano wa shirikisho hilo kwa kuunda kamati ya maadili ya kujitegemea ili kuchunguza na kutoa adhabu kwa wale watakaogundulika kushiriki vitendo vya rushwa. Baada ya FIFA kukumbwa na kashfa za rushwa katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011, shirikisho hilo liliongezea nguvu katika kamati ya maadili kwa kuigawanyisha mara mbili, moja ikiwa ni kufanyia uchunguzi kesi zinazohusiana na masuala hayo na nyingine kwa ajili ya kutoa hukumu na adhabu. Blatter amesema FIFA pekee haiwezi kusimamia watu wapatao milioni 300 duniani kote wanaohusika katika soka ndio maana anataka mashirikisho ya soka barani kote kuongezea nguvu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)


