Friday, February 1, 2013
FIFA PEKEE HAIWEZI KUPAMBANA NA VITENDO VYA RUSHWA KWENYE SOKA - BLATTER.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter amesema kuwa vita dhidi ya vitendo vya rushwa katika mchezo wa soka haviweza kupiganwa na wao pekee bali pia mashirikisho kutoka pande zote duniani inabidi watoe ushirikiano. Blatter anaamini kuwa wanachama 209 wa FIFA pamoja na mashirikisho ya mabara wanatakiwa kufuata mfano wa shirikisho hilo kwa kuunda kamati ya maadili ya kujitegemea ili kuchunguza na kutoa adhabu kwa wale watakaogundulika kushiriki vitendo vya rushwa. Baada ya FIFA kukumbwa na kashfa za rushwa katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011, shirikisho hilo liliongezea nguvu katika kamati ya maadili kwa kuigawanyisha mara mbili, moja ikiwa ni kufanyia uchunguzi kesi zinazohusiana na masuala hayo na nyingine kwa ajili ya kutoa hukumu na adhabu. Blatter amesema FIFA pekee haiwezi kusimamia watu wapatao milioni 300 duniani kote wanaohusika katika soka ndio maana anataka mashirikisho ya soka barani kote kuongezea nguvu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment