Friday, February 1, 2013
MUSTAKABALI WA KAKA MASHAKANI.
MUSTAKABALI wa kiungo wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Real Madrid, Kaka unaonekana kuwa mashakani baada ya uhamisho wake katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kushindikana huku kocha wake Jose Mourinho akimuondoa katika kikosi chake cha kwanza. Kaka mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia mwaka 2007 ambaye aliigharimu Madrid kiasi cha euro milioni 65 wakati aliponunuliwa akitokea Ac Milan mwaka 2009 hatakuwepo hata kwenye benchi la wachezaji wa akiba wakati wa mechi ya La Liga dhidi ya Granada baadae leo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwemo katika benchi ya wachezaji wa akiba katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mfalme waliotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Barcelona Jumatano iliyopita lakini hakupata nafasi ya kuingia. Mambo yamekuwa hayamuendei vyema mchezaji huyo toka Mourinho atue klabuni hapo akiwa ameanza mara 11 pekee katika mechi za La Liga, mara mbili katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na maa moja katika Kombe la Ligi. Kulikuwa na tetesi kuwa nyota huyo angeweza kurejea katika klabu yake ya zamani ya Milan lakini muda wa kufungwa kwa dirisha hilo hakuna makubaliano yoyote yaliyofikia huku kikubwa kilichokwamisha mpango kikiwa ni mshahara mkubwa wa mchezaji huyo anaoupokea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment