Friday, February 1, 2013
BALOTELLI APONDA MAISHA YA UINGEREZA.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Italia mwenye vituko vingi, Mario Balotelli amesema anajisikia faraja kuondokana na vyombo vya habari, kuendesha, hali ya hewa pamoja na vyakula vya Uingereza wakati akisaini rasmi kuiwakilisha klabu ya Ac Milan ya Italia. Balotelli ambaye wakati akiwa Uingereza amekuwa akipata adhabu za mara kwa mara kutokana na aina ya uendeshaji wake, aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuichezea Milan ilikuwa ni ndoto alizokuwa nazo siku nyingi na amefurahi kuwepo hapo. Nyota huyo mwenye miaka 22 amesema amefurahi kurejea karibu na familia na marafiki zake baada ya kuiacha klabu yake ya Manchester City ambayo amekuwa akiingia mizozo ya mara kwa mara na kocha wake Roberto Mancini. Balotelli ambaye amesajiliwa na Milan kwa ada ya euro milioni 20 amesema kuna baadhi ya mambo atakayokumbuka wakati alipokuwa mojawapo ni wakati wa kwenda mazoezini huko Carrington akiwa na wachezaji wenzake pamoja na kocha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment