Monday, June 8, 2015

BAADA YA MILNER, SASA LIVERPOOL WAMNASA INGS.

KLABU ya Liverpool, imethibitisha kuwa tayari wameshanasa saini ya mshambuliaji wa Burnley Danny Ings. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza, ameshamaliza mkataba wake na Burnley na anatarajiwa kutua Anfield Julai mosi baada ya kufanyiwa vipimo vya afya. Ings mwenye umri wa miaka 22, amefunga mabao 11 katika Ligi Kuu msimu huu lakini hakuweza kusaidia timu yake hiyo kutoshuka daraja. Nyota huyo wa zamani wa Bournemouth yuko katika kikosi cha Uingereza cha vijana chini ya umri wa miaka 21 kea ajili ya michuano ya ubingwa ya Ulaya baadae mwezi huu huko Jamhuri ya Czech. Ings anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Liverpool baada ya James Milner kujiunga nao akitokea Manchester City wiki iliyopita.

MOURINHO AKIRI KUSAKA MSHAMBULIAJI MPYA CHELSEA.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amebainisha kuwa klabu hiyo itaingia sokoni katika usajili huu wa majira ya kiangazi kutafuta mshambuliaji mpya. Wiki iliyopita kulizuka tetesi kuwa Mourinho alikuwa akitaka kumsajili Radamel Falcao ambaye ameshindwa kung’aa katika Ligi Kuu toka alipochukuliwa kea mkopo na Manchester United kiangazi mwaka jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia tayari amesharejea katika klabu yake ya Monaco baada ya United kuamua kutomnunua pamoja na kuwa na nafasi ya kufanya hivyo. Akihojiwa Mourinho amesema wanataka kununua mshambuliaji kwasababu wanahitaji kuwa na washambuliaji watatu walio katika kiwango bora. Hata hivyo, Mourinho hakuweka wazi na mshambuliaji yupi anayemuhitaji na kudai kuwa wana chaguo zaidi ya moja.

KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA SASA LAFIKIA HATUA YA MAKUNDI.

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Al Ahly ya Misri wamefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo kea ushindi wa matuta dhidi ya Club Africain ya Tunisia. Club Africain walifanikiwa kushinda mchezo huo wa maruadiano wa mtoano kea mabao 2-1 na kugeuza matokeo kuwa sare ya mabao 3-3 baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza. Sare hiyo ilipelekea mchezo huo kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Al Ahly waliibuka kidedea kea kufunga penati 5-4. Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo, CS Sfaxien wao walikuwa na bahati kuliko wa Tunisia wenzao baada ya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast. Katika michezo mingine Etoile du Sahel walifanikiwa kugeuza matokeo ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza na kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa meridian dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco na kuifanya kuwa timu ya tatu kutoka Tunisia kuingia hatua ya makundi. Mabingwa wa zamani wa Afrika Zamalek ya Misri pia nao walifanikiwa kugeuza matokeo ya kufungwa mechi ya mkondo wa kwanza na kushinda mabao 3-1 nchini Misri dhidi ya Sanga Balende ya DR Congo hivyo kusonga mbele lwa jumla ya mabao 3-2. Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini wao waliingia hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa kishindo baada ya kuitabdika AS Kaloum ya Guinea kea mabao 4-1 katika mchezo wa maruadiano uliofanyika Soweto hivyo kusonga mbele kea jumla ya mabao 6-1.

LEBRON JAMES AIBEBA CAVALIERS KATIKA FAINALI YA PILI NBA.

MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu wa Cleveland Cavaliers, LeBron James ameisaidia timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa vikapu 95-93 dhidi ya Golden State Warriors na kufanya timu hizo kwenda sare ya kufungana mchezo mmoja mmoja katika fainali ya pili ya NBA. Katika mchezo huo James alifanikiwa kufunga vikapu 39, kudaka rebound 16 na kutoa pasi za mwisho 11. Akihojiwa James mwenye umri wa miaka 30, amesema alijitahidi kufanya kila analoweza kwa ajili ya timu na anashukuru kea ushirikiano aliopata kutoka kea wachezaji wenzake na kuepelekea kufanikisha ushindi huo muhimu. Katika fainali ya kwanza kati ya saba ambazo timu hizo zitacheza, Warriors walifanikiwa kuibuka na ushindi wa vikapu 108-100.

PIRLO AKANUSHA KUONDOKA JUVENTUS.

KIUNGO mahiri wa Juventus, Andrea Pirlo amesisitiza kuwa machozi yaliyomtoka baada ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yalikuwa in kutokana na matokeo na sio kwamba alikuwa akiaga. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia amewahi kukiri huko nyuma kuwa angependa kuondoka Turin kama Juventus wangeifunga Barcelona jijini Berlin pamoja na kuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Hata hivyo, wakati mkongwe huyo akimwaga chozi baada ya kutandikwa mabao 3-1 na Barcelona, wachambuzi wengi wa soka walioanisha tukio hilo na nia yake ya kutaka kuondoka. Akihojiwa Pirlo amesema sio kweli kwanza alilia kwasababu mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwake bali matokeo waliyopata ndio yaliyokuwa yakimhuzunisha.

Saturday, June 6, 2015

BARCELONA MFALME ULAYA.

KLABU ya Barcelona wametawadhwa mabingwa wapya wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana baada ya kuibuka kidedea katika mchezo wa fainali dhidi ya mabinga wa Italia Juventus uliofanyika katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin, Ujerumani.Mabao mahiri yaliyofungwa na Ivan Rakitic katika dakika ya nne, Luis Suarez dakika ya 68 na Neymar dakika ya tisini yalitosha kuihakikishia Barcelona taji lake la sita la michuano hiyo kwa kushinda mabao 3-1.
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo meneja wa Barcelona Luis Enrique pamoja na kubainisha kuwa hajui mustakabali wake lakini amefurhishwa na mafanikio hayo ya muda mfupi aliyopata toka alipochukua kibarua hicho kutoka Gerardo Martino kiangazi mwaka jana.Naye meneja wa Juventus Massimiliano Allegri alikiri kuzidiwa maarifa na wapizania wao lakini amedai kuwa atajipanga vyema kuimarisha kikosi chake il msimu ujao waweze kutoa upinzani mkali zaidi.

SERENA AENDELEA KUTAMBA TENISI WANAWAKE.

MWANADADA nyota wa tenisi wa Marekani Serena Williams ametawadhwa bingwa mpya wa michuano ya wazi ya Ufaransa baada ya kuibuka mshindi katka mchezo wa fainali dhidi ya Lucie Safarova.Williams mwenye umri wa miaka 33, alishinda taji hilo la tatu kwake kwa michuano hiyo kwa seti 2-1 zenye alama za 6-3 6-7 6-2.Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Williams alikiri kuwa michuano hiyo ilikuwa migumu kwake kwakuwa alicheza muda mwingi akiwa hayuko fiti kiafya asilimia mia moja.Kwa upande wa wanaume Novak Djokovic aliibuka kidedea na kutinga fainali ya michuano hiyo kwa kumchapa Andy Murray wa Uingereza katika mchezo ulioamuliwa kwa seti tano.Katika mchezo huo ulioanza Ijumaa na kukatishwa na hali mbaya ya hewa, Djokovic alishinda kwa alama 6-3 6-3 5-7 5-7 6-1, ambapo sasa atakwaana na Stan Wawrinka katika hatua ya fainali baadae.