MCHEZAJI tenisi namba moja duniani kwa upande wa wanawake, Serena Williams anatarajia kujaribu kushinda taji la sita la michuano ya WTA Miami Masters inayoendelea huko nchini Marekani. Katika michuano hiyo ambayo zawadi yake ni kitita cha dola milioni 8.5, Williams anatarajiwa kupambana na Flavia Pennetta katika mzunguko wa pili wa michuano hiyo baada ya mwanadaa huyo anayeshika namba 103 katika orodha za ubora kumfunga Johanna Larson wa Sweden kwa 6-4 6-1. Kama Williams akifanikiwa kutinga mzunguko wa tatu kwa kumfunga Pennetta anaweza kukutana na Yahina Wickmayer wa Ubelgiji au Ayumi Morita wa Japan ambaye alimuondosha Heather Watson wa Uingereza kwa 1-6 7-5 6-4. Williams mwenye umri wa miaka 31 anayeshikilia mataji 15 ya Grand Slam amewahi kushinda michuano ya Miami mwaka 2002, 2003, 2004, 2007 na 2008 huku akifika hatua ya fainali katika michuano ya 1999 na 2009. Dada yake Williams ambaye anashika namba 19 katika orodha za ubora Venus anatarajia kuanza kampeni zake kwa kupambana na Kimiko Date-Krumm wa Japan wakati bingwa mtetezi wa michuano hiyo Agnieszka Radwanska wa Poland anatarajiwa kuanza na Hsieh Su-Wei wa Taiwan.
Wednesday, March 20, 2013
TAARIFA KUTOKA TFF LEO.
KIKOSI CHA MOROCCO KUTUA NCHINI IJUMAA
Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency. Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri. Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira. Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi. Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.
Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili mchana.

BRAZIL WANA UWEZO WA KUANDAA MICHUANO YA KUVUTIA - BLATTER.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter anaamini kuwa Brazil ina nguvu za kutosha kiuchumi kwa ajili ya kuandaa michuano ya kihistoria ya Kombe ya Dunia 2014. Kauli hiyo ya Blatter mwenye umri wa miaka 77 ameitoa mara baada ya kufanya kikao na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Aldo Rebelo kuzungumzia maendeleo ya ujenzi wa viwanja na miundo mbinu mingine kwa ajili ya michuano hiyo. Akihojiwa na mtandao wa shirikisho hilo Blatter amesema ana uhakika wa asilimia mia moja kwamba Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia watakuwa tayari kwa ajili michuano hiyo kwa wakati. Mbali na kauli hiyo ya Blatter FIFA pia ilitangaza tarehe ya kufanyika sherehe za upangaji ratiba wa michuano hiyo ambayo itakuwa ni Desemba 6 mwaka huu katika hoteli ya Costa do Sauipe iliyopo katika jimbo la Bahia.
Tuesday, March 19, 2013
OWEN ATANGAZA KUTUNDIKA DARUGA.
MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Michael Owen ametangaza leo kustaafu rasmi soka ifikapo mwishoni mwa msimu huu. Owen mwenye umri wa miaka 33 alitangza azma yake hiyo katika mtandao wake binafsi kwa kudai kuwa anadhani wakati umefika wa kutundika daruga zake. Nyota huyo alianza kucheza katika kikosi cha kwanza Liverpool akiwa na umri wa miaka 17 na pia amewahi kucheza katika vilabu vya Real Madrid, Newcastle United, Manchester United na klabu yake ya sasa Stoke City. Mshambuliaji huyo ambaye amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya mwaka 2001 amecheza mechi 89 za kimataifa akiwa na kikosi cha Uingereza na kufunga mabao 40 lakini maisha yake ya soka yamekuwa katika misukosuko kutokana na majeruhi ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakimsumbua. Owen aliwashukuru wale wote ambao wamekuwa karibu yake wakiwemo wachezaji, makocha na marafiki zake katika kipindi chote alichokuwa akicheza.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
KIINGILIO MECHI YA STARS, MOROCCO 5,000/-
Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani. Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni sh. 10,000. Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000. Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku mbili ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala.
Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Vilevile tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo.
SAMATA, ULIMWENGU WARIPOTI STARS

Washambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili nchini jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini. Ujio wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mcha aliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti kambini leo asubuhi. Wachezaji John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao walikuwa Liberia na timu yao ya Azam wataripoti kambini leo alasiri. Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia nayo wenzao kuwa imejaa. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha Kim Poulsen leo inaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa. Mazoezi hayo yataanza saa 9 alasiri.
TIMU TATU ZASHUKA DARAJA FDL
Timu tatu zimeshuka daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kurudi Ligi ya Mkoa msimu ujao wa 2013/2014 baada ya kushika nafasi za mwisho katika ligi hiyo msimu huu 2012/2013 iliyomalizika wikiendi iliyopita. Small Kids ya Rukwa imeporomoka kutoka kundi A baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo mapema kwa kushindwa kufika uwanjani kwenye moja ya mechi zake. Kwa mujibu wa kanuni matokeo yote ya mechi ilizocheza yalifutwa. Moro United ya Dar es Salaam ndiyo iliyoaga FDL kutoka kundi B baada ya kumaliza mechi zake ikiwa na pointi tatu. Wakati kutoka kundi C timu iliyoshuka ni Morani ya Manyara iliyomaliza ligi ikiwa na pointi kumi na moja. Timu zilizopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2013/2014 ni Mbeya City ya Mbeya iliyoongoza kundi A ikiwa na pointi 31, vinara wa kundi B timu ya Ashanti United ya Dar es Salaam yenye pointi 29 wakati Rhino Rangers ya Tabora imepanda kutoka kundi C ikiwa na pointi 32.
LIUNDA KUTATHIMINI WAAMUZI KOMBE LA DUNIA
Mwamuzi Msaidizi wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathimini wa waamuzi (referee assessor) kwenye moja ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia. Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Liunda kutathimini waamuzi kwenye mechi kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Libya itakayochezwa Jumapili (Machi 24 mwaka huu). Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Martyrs jijini Kinshasa kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika ya Kati (CAT). Waamuzi watakaochezea mechi hiyo William Selorm Agbovi atakayekuwa mwamuzi wa kati, Malik Alidu Salifu (mwamuzi msaidizi namba moja), David Laryea (mwamuzi msaidizi namba mbili) na mwamuzi wa mezani (fourth official) Cecil Amatey Fleischer. Waamuzi wote hao wanatoka Ghana.

TIGER WOODS AVUTA KIFAA KIPYA.
NYOTA namba moja wa zamani duniani katika mchezo wa gofu, Tiger Woods na bingwa wa michuano ya olimpiki ya kuteleza kwenye barafu wa Marekani Lindesey Vonn wametangaza rasmi kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Wawili hao walitangaza taarifa hizo katika kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo walituma picha wakiwa pamoja na kumaliza uvumi uliokuwa umesambaa juu ya mahusiano yao. Woods amewahi kumuoa mwanamitindo kutoka Sweden Elin Nordegrem lakini walitalikiana mwaka 2010 baada ya nyota huyo tajiri kukiri kuwa na mahusiano na wanawake mbalimbali akiwa ndani ya ndoa yao. Woods mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akihangaika kurejea katika kiwango chake toka kipindi hicho na sasa ameanza kuonyesha dalili za kurejesha makali yake ambayo yalimfanya atawale mchezo wa gofu kwa muongo mmoja.
KUNDI LA NYUKI LATISHIA KUSIMAMISHA MCHEZO BRAZIL.
MWISHONI mwa wiki iliyopita kundi ya nyuki ambao hawakujulikana walipotokea kidogo wazuie mchezo wa Ligi Kuu nchini Brazil usichezeke baada ya kujikusanya kundi katika mlingoti wa goli. Mchezo huo kati ya timu ya Ponte Preta na Atletico Sorocaba uliingia katika msukosuko huo baada ya kundi la nyuki kujikusanya katika mlingoti wa goli la Uwanja wa Moises Lucarelli na kadri muda wa kuanza pambano hilo ulipokuwa ukisogea ndivyo kundi la nyuki hao lilivyozidi kuongezeka na kuwa kubwa. Baadhi ya picha zilizopigwa uwanjani zinawaonyesha watu wa kikosi cha zimamoto waliovaa mavazi maalumu wakipanda katika ngazi kabla ya kuwapulizia mitungi ya kuzimia moto na baada ya kupuliza hewa ya petrol kuzunguka eneo hilo kabla ya mchezo huo kuanza. Kuchelewa kwa mechi hiyo ilikuwa ni faida ya wenyeji Ponte Preta ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuendelea kung’ang’ania katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi ya nchi hiyo wakiwa na alama sawa na vinara Sao Paulo baada ya michezo 12 kuchezwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)