BRAZAVILLE, Gabon.
NAHODHA wa Cameroon Samuel Eto'o na Rais wa Gabon Ali Bongo Jumatano walianza ziara ya maeneo tofauti katika miji ya Libreville na Franceville ambapo ujenzi unaendelea ikiwa ni maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika 2012.
Gabon ni muandaaji mwenza pamoja na jirani yake Equatorial Guinea, lakini maandalizi ya Gabon yamekuwa yakisuasua na watu wamekuwa na mashaka kama kazi hiyo itakwisha kwa muda stahiki.
Picha za mshambuliaji huyo wa Inter akiwa amevaa kofia ngumu pamoja na koti huku akiwa pembeni mwa Rais zilionyeshwa katika luninga ya taifa ya nchi hiyo Alhamisi.
Baada ya kutembelea Fanceville ambao ni mji wa pili kwa ukubwa katika nchi hiyo Jumatano, ugeni huo ulielekea Brazaville ambapo walitembelea Hospitali ya rufaa, Uwanja Omar Bongo, sehemu ya vifaa vya mazoezi na Hoteli ya Nzeng Ayong.
Michuano hiyo ambayo ni ya 28 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Januari 21 hadi Februari 12 mwaka kesho.

No comments:
Post a Comment