Kocha wa Taifa Stars Jan Poulsen. |
DAR ES SALAAM, Tanzania
KIUNGO wa Simba Haruna Moshi 'Boban' ambaye alionyesha kiwango kizuri katika michuano ya Kombe la Cecafa anaweza kupewa nafasi nyingine katika timu ya Taifa na Kocha wa timu hiyo Jan Poulsen.
Boban atarejeshwa katika timu ya Taifa baada ya kukacha kikosi cha timu ya Taifa vijana chini ya miaka 23 siku kadhaa zilizopita.
"Ligi Kuu karibu inaanza na nitaangalia maendeleo yake kwa karibu. Pengine naweza kumjumuisha katika kikosi changu kitakachocheza na Algeria," alisema Poulsen akiongea na gazeti moja hapa nchini.
Haruna Moshi "Boban" |
"Kila mchezaji ana haki ya kuchezea timu yake ya Taifa lakini makocha wanaangalia ubora pamoja na tabia nzuri. Kama Boban atakuwa navyo hivyo vitu lazima atakuwa katika kikosi changu." alimalizia Poulsen.
Boban ni mmoja kati ya wachezaji watatu walioenguliwa na kocha wa zamani wa taifa Stars Marcio Maximo wakati wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Chan, ambapo wengine ni Athmani Iddi 'Chuji' na Amir Maftah.
No comments:
Post a Comment