BEKI wa klabu Manchester United Patrice Evra amemwambia kocha wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson kuwa ameamua kumshitaki mshambuliaji waLiverpool Luis Suarez kwa vitendo vya kibaguzi alivyomfanyia.
Evra alitoa tuhuma hizo dhidi ya mchezaji huyo baada ya mchezo uliozikutanisha timu hizo katika Uwanja wa Anfield Jumamosi iliyopita ambapo timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Hata hivyo Evra anaamini kuwa picha za televisheni ndizo zitazotoa ushahidi wa yeye kufanyiwa tukio hilo, Suarez alikana tukio hilo na kusema kuwa amechukizwa tuhuma hizo dhidi yake.
Akihojiwa kuthibisha kama kweli ameongea na mchezaji huyo Ferguson alikiri ni kweli waliongea kuhusu hilo na ameamua kulifuatilia hilo.
No comments:
Post a Comment