MISRI imejitoa kuandaa michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki mashindano ya Olympic.
Michuano hiyo yenye timu nane yalipangwa kuchezwa jijini Cairo kuanznia Novemba 26 mpaka Desemba 10 waka huu.
Timu tatu za juu ndizo zitakazoiwakilisha bara kwa ajili mashindano ya Olympic yatakayofanyika jijini London, Uingereza mwakani.
Misri tayari wamelifahamisha Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuhusu uamuzi wake huo.
Chama cha Soka cha nchi hiyo kimetoa uamuzi huo kutokana tatizo la usalama lilipo hivi sasa pamoja na uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Novemba.
Pamoja na Misri timu zingine zinazotarajiwa kushiriki katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Algeria, Gabon, Ivory Coast, Morocco, Nigeria, Senegal na Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment