MSHAMBULIAJI wa Arsenal Robin van Persie huenda akaongezewa mkataba mrefu na na klabu yake hiyo ili kumbakisha mchezaji tegemeo.
Mchezaji huyo wa Kimataifa kutoka Uholanzi majaliwa yake ya kuwepo klabuni hapo yapo mashakani baada kukiri kuwa hahitaji kuongelea suala la mkataba mpya kwa hivi sasa mpaka msimu utapomalizika. Lakini Arsenal wako tayari kuvunja utaratibu wao wa malipo kwa wachezaji ili kuhakikisha wanampakisha nyota huyo.
Mkataba wa Van Persie unakwisha 2013 na Arsenal wanahitaji kumsainisha mkataba kabla ya msimu kumalizika. Klabu hiyo iliwapoteza nyota wake Samir Nasri na Gael Clichy mwaka huu baada kushindwa kufikia makubaliano hivyo hawataki hilo litokee kwa Van Persie.
Mchezaji huyo kwasasa analipwa paundi 70,000 kwa wiki lakini chanzo kimoja cha habari kutoka klabuni hapo kilitonya kuwa anaweza kuongezewa kiasi kikubwa zaidi ili kumbakisha. Nasri alikataa mshahara wa paundi 90,0000 kwa wiki na kujiunga na Manchester City na Arsenal wanaweza kumuongezea kiasi kama hicho mchezaji huyo.
Pia anaweza kupewa mkataba wa miaka minne kitu ambapo kitakwenda kinyume na sera za klabu za kumpata mchezaji ambaye anakaribia miaka 30 mkataba mrefu kama huo.
Kwa miaka mingi Arsenal wamekuwa mkataba wa mwaka mmoja mmoja kwa wachezaji walio na umri wa miaka 30 au zaidi, hata hivyo Kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger amevunja mwiko huo baada ya kumsainisha beki Sebastian Squillaci mkataba wa miaka mitatu ingawa ana miaka 30 na mchezaji kutoka Sevilla Mikel Arteta ambaye amepewa miaka mkataba wa miaka minne wakati anatimiza umri wa miaka 30 Machi mwakani.
Akiongea wiki iliyopita, Mtendaji Mkuu Ivan Gazidis alidokeza kuwa klabu hiyo ipo tayari kubadili utaratibu wake wa malipo ili kuwabakisha nyota wake.
No comments:
Post a Comment