Saturday, October 29, 2011

SIMBA, YANGA HAPATOSHI LEO. CHELSEA, ARSENAL NAO VITANI.


MACHO na masikio ya watanzania yataelekea katika Uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam ambapo mtanange wa kukata na shoka katika mahasimu wawili Simba na Yanga zitakapochuana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Simba ambao wanaongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 27 katika michezo 11 waliyocheza wataingia uwanjani huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wa kwanza wa ngao ya jamii dhidi ya watani wa jadi.Yanga ambaye ni bingwa mtetezi wa ligi hiyo wenyewe walianza ligi hiyo kwa kusuasua kabla ya kuzinduka kipindi cha hivi karibuni wako katika nafasi ya pili mwa msimamo wakiwa wamejikusanyia pointi 21 katika michezo 11 waliyocheza hivyo mchezo huu utakuwa ni muhimu kwao kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lake.

Na kimataifa huko Uingereza wapenzi wa soka wataelekeza masikio yao katika Uwanja wa Stamford Bridge ambapo Chelsea wataikaribisha Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kuvutia.Mbali na mchezo huo michezo mingine itakayochezwa leo itakuwa, Everton itaikaribisha Manchester United, Manchester City na Wolveshampton, Norwich na Blackburn, Sunderland na Aston Villa, Swansea na Bolton, wigan na Fulham wakati West Bromwich wataikaribisha Liverpool.

No comments:

Post a Comment