Friday, October 28, 2011

WENGER AKIRI KUTETA NA VAN PERSIE KUHUSU MKATABA MPYA.

KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger ameiambia BBC, klabu hiyo imeanza mazungumzo na Robin van Persie kuhusiana na mkataba mpya.
Van Persie, ambaye ni nahodha wa klabu hiyo, tayari ameshapachika mabao 13 katika mechi zote ilizocheza Arsenal msimu huu na mkataba wake wa sasa unamalizika mwezi wa Julai 2013.
Alipoulizwa moja kwa moja iwapo anafanya mazungumzo na Van Persie, Wenger alikubaliana na sula hilo.
Amesema mchezaji huyo amebakisha miezi 18 kabla ya mkataba wake wa sasa kufikia ukingoni na ana uhakika atasaini mkataba mpya.
Van Persie ndiye mchezaji pekee wa Arsenal aliyebakia katika kikosi hicho ambaye aliyewahi kushinda kikombe akiichezea timu hiyo.
Wenger anatarajiwa kufanya kila awezalo kumbakisha mpachika mabao wao huyo hodari baada ya kuondoka msimu huu wachezaji muhimu Samir Nasri, Cesc Fabregas na Gael Clichy.
Hata hivyo, Wenger alifanikiwa kuwachukuwa wachezaji wawili wa kiungo Yossi Benayoun na Mikel Arteta, wakati mlinzi Per Mertesacker na mshambuliaji Ju-Young Park pia waliongezwa katika kikosi cha timu hiyo.

No comments:

Post a Comment