Friday, October 28, 2011

REBELO WAZIRI MPYA WA MICHEZO BRAZIL.

Aldo Rebelo
RAIS wa Brazil Dilma Rousseff amemtua Aldo Rebelo kuwa Waziri mpya wa Michezo wa nchi hiyo akiziba nafasi ya Orlando Silva aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya rushwa inayomkabili.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo ilisema kuwa Rebelo ndio atakuwa mwkilishi wa serikali katika maandalizi ya Kombe la Dunia 2014 na michuano ya Olympic itakayofanyika 2016.
Rebelo aliitumikia serikali ya zamani iliyokuwa ikiongozwa na rais Luiz Inacio Lula da Silva kama waziri anayeshughulikia mambo ya kisiasa na mahusiano ya taasisi mwaka 2004 na 2005.
Silva alijiuzulu wadhifa wake huo Jumatano baada ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo kuamrisha uchunguzi ufanyike juu ya sakata hilo. Silva alipinga tuhuma hizo mbele ya mkutano wa bunge la nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment