Friday, October 28, 2011

SABELLA AITA 21 WA KUIVAA COLOMBIA.

Alejandro Sabella
KOCHA wa timu ya Taifa ya Argentina Alejandro Sabella amemuita kiungo Fernando Gago na Pablo Guinazu kwa mara ya kwanza anayechezea timu ya Internacional ya Brazil kwa ajili michezo ya kutafuta tiketi ya kuchezo michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Bolivia na Colombia inayoarajiwa kuchezwa mwezi ujao.Kocha huyo ambaye timu yake iliifunga Chile mabao 4-1 nyumbani kabla ya kufungwa na Venezuela bao 1-0 ugenini mapema mwezi huu aliwaita wachezaji hao katika kikosi cha wachezaji 21 wa timu hiyo Alhamisi hii.
Kikosi kamili cha timu hiyo na vilabu wanavyochezea katika mabano ni Makipa Sergio Romero (Sampdoria), Mariano Andujar (Catania), Mabeki watakuwa Martin Demichelis (Malaga), Nicolas Burdisso (AS Roma), Federico Fernandez (Napoli), Luciano Monzon (Nice), Pablo Zabaleta (Manchester City), Marcos Rojo (Spartak Moscow).Wakati viungo watakuwa Javier Mascherano (Barcelona), Ever Banega (Valencia), Fernando Gago (AS Roma), Javier Pastore (Paris St Germain), Nicolas Gaitan (Benfica), Jose Sosa (Metalist Kharkiv), Pablo Guinazu (Internacional) na washambuliaji watakuwa Lionel Messi (Barcelona), Angel Di Maria, Gonzalo Higuain (wote Real Madrid), Ezequiel Lavezzi (Napoli), German Denis (Atalanta), Sergio Aguero (Manchester City).

No comments:

Post a Comment