Saturday, October 29, 2011

BAFANA BAFANA KUKIPIGA NA IVORY COAST KOMBE LA MADIBA.


TIMU ya Taifa ya Afrika Kusini-Bafana Bafana inatarajiwa kupambana na Ivory Coast katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa Kombe la Nelson Mandela Novemba 12 mwaka huu katika Uwanja wa Nelson Mandela Bay, Port Elizabeth.

Ofisa Mkuu wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-SAFA- Robin Petersen alithibitisha timu hiyo itapambana na timu ngumu ya Ivory Coast ambayo itakuwa na nyota wake wanaocheza nje Ulaya kama Didier Drogba na Salomon Kalou wanacheza Chelsea, Kolo Toure na mdogo wake Yaya wanacheza Manchester City na Gervinho anayekipiga Arsenal.

Naye Rais wa SAFA Mwelo Nonkonyana amesema kuwa anaamini mchezo huo utawafuta machozi mashabiki wa soka wa nchi hiyo baada ya kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika mapema mwaka kesho.

Timu ya Ivory Coast ambayo iliiwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia mwaka 2006 na 2010 ndio inayopigiwa chapuo kunyakuwa ubingwa wa michuano hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya Equatorial Guinea na Gabon.

No comments:

Post a Comment