Saturday, October 29, 2011

TOURE KIKAANGONI TENA.


MLINZI wa Manchester City Kolo Toure ataikabili kamati ya nidhamu ya klabu hiyo wiki ijayo kuhusiana na suala la kugundulika alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu mapema mwaka huu.
Tume binafsi ya nidhamu mwezi wa Mei ilimfungia Toure kucheza kandanda kwa muda wa miezi sita, ingawa shauri hilo lilitokea tangu mwezi wa Machi, baada ya vipimo alivyofanyiwa kuonesha alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu ambazo zimekatazwa.
Tangu aliporejea uwanjani mwezi wa Septemba ameshacheza mechi nne.
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ataendelea kubakia katika ushindani mkubwa kuweza kupata nafasi ya kucheza.
Kusikilizwa kwa shauri hilo kulicheleweshwa hadi sasa kwa sababu wajumbe wa kamati hiyo ya sheria walishindwa kupanga tarehe muafaka.
Mchezaji mwenzake Toure, Carlos Tevez, ambaye alipatikana naonekana na hatia ya kukiuka vifungu vitano vya mkataba wake wiki hii, alifanya mazoezi mbali na wachezaji wa kikosi cha kwanza na hajacheza mechi yoyote ya maana wakati shauri lake lilipokuwa likiendelea likisikilizwa.
Lakini Mancini amesema suala la Toure ni tofauti. Ilikuwa ni makosa..
Toure, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2013, alisimamishwa kucheza soka baada ya kutumia dawa za kupunguza uzito za mkewe.
Alifanyiwa vipimo mwezi wa Februari wakati Manchester City ilipopambana na Manchester United ambapo alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakucheza, na alisimamishwa tarehe 3 mwezi wa Machi baada ya sampuli kuonesha ametumia dawa zilizokatazwa.

No comments:

Post a Comment