Thursday, November 10, 2011

ADEBAYOR AREJEA TOGO.

HATIMAYE mshabuliaji wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor amerejea tena katika kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo baada ya kutangaza kustaafu mapema mwaka jana. Adebayor-27 alikubali kurejea katika kikosi hicho baada ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo kumhakikishia usalama wakati walipokutana jana kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa shirikisho hilo. Mshambuliaji anayechezea klabu ya Tottenham Hotspurs amesema amefurahi kurejea na kuwa atakuwepo katik kikosi cha timu hiyo kitachopambana na Guinea Bissau katika kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014.
Adebayor alistaafu kuichezea Togo baada ya tukio la kushambuliwa kwa risasi basi lao katika mji wa Cabinda wakielekea katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka jana ambapo watu wawili walikufa na golikipa wao Kojovi Obilale kujeruhiwa vibaya.

No comments:

Post a Comment