Monday, November 28, 2011

"BARCELONA BADO INA NAFASI YA KUNYAKUWA LA LIGI." CRUYFF.

MCHEZAJI nguli wa zamani wa Barcelona Johan Cruyff amewashangaa watu wanaodai kuwa timu hiyo haiwezi kutetea ubingwa wake wa La Liga msimu huu. Wakati akihojiwa na waandishi kabla ya mchezo kati ya timu ya hiyo na Esperance ya Tunisia Cruyff amesema kuna mataji manne msimu huu na Barcelona hawajalipoteza lolote mpaka sasa hivyo haoni sababu ya watu kuibeza timu hiyo kwasasa. Barcelona imepotza mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa Getafe baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 Jumamosi iliyopita hivyo kuwa nyuma katika nafasi ya pili wakiwa na tofauti ya alama sita nyuma ya vinara wanaoongoza ligi hiyo Real Madrid. Mchezaji huyo wa zamani ambaye kwasasa ana umri wa miaka 64 amesema kuwa watu wengi inaonekana hawajui ubora wa timu ya Barcelona na sio kwamba mambo yanakwenda vibaya kwasababu wamefungwa huo mchezo mmoja.

No comments:

Post a Comment