Monday, November 28, 2011
WAZIRI MKUU BULGARIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA MCHEZAJI BORA.
WAZIRI Mkuu wa Bulgaria Boiko Borisov yuko mbioni kuitwa katika orodha ya mchezaji bora wa mwaka wan chi hiyo baada ya mshambuliaji wa Manchester United kuchoka kushinda tuzo hiyo mara kwa mara. Borisov akipata nafasi huwa anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya daraja la tatu ya Vitosha Bistritsa ambayo kwa jina la utani inatambulika kama Tigers na mpaka sasa anaongoza kwa kura 2000 zilizopigwa na mashabiki kumuingiza katika orodha hiyo. Akihojiwa Borisov mwenye miaka 52 amesema hakuna mtu yoyote anayeweza kumwambia kwamba yeye ni mchezaji mbovu na kuisifia timu yake ya Tigers kuwa ni timu bora. Hii ni mara ya kwanza kwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo kuruhusu mashabiki kushiriki katika mchakato huo ambapo watateua orodha ya wachezaji 20 watakaoshindanishwa wakati kura za mwisho zitapigwa na waandishi wa habari. Waziri Mkuu huyo mbali ya kuwa mshambuliaji hodari pia ana mkanda mweusi katika sanaa ya mapigano ya karate na mchezaji mzuri wa mchezo wa tenisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment