Saturday, November 5, 2011

BECKHAM ATAKA KOCHA MZAWA WAKUIFUNDISHA UINGEREZA.

DAVID Beckham amedai wakati umefika kwa timu ya Taifa ya Uingereza kunolewa na raia wa nchi hiyo baada ya Fabio Capello kubwaga manyanga baada ya michuano ya Ulaya mwaka 2012. Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza amesema kwa kipindi kirefu hawajapata kocha mzawa, hivyo waingereza wanahitaji kocha mzawa katika kipindi kijacho. Beckham pia amemtetea mshambuliaji wa Manchester United na kudai kuwa ni lazima ajumuishwe katika kikosi cha nchi hiyo kitachokwenda katika michuano hiyo ya Ulaya. Amesema kama timu hiyo itafanikiwa kuvuka hatua za mwanzo itakuwa ni wakati muafaka Rooney kuitumikia timu hiyo. kwasasa mchezaji huyo amefungiwa mechi tatu na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA baada ya kumchezea vibaya Miodrag Dzudovic wa Montenegro mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment