Saturday, November 5, 2011
FA KUMKATIA RUFANI ROONEY.
SHIRIKISHO la Soka nchini (FA) wameamua kukata rufani dhidi ya adhabu ya kufungiwa kwa mechi tatu aliyopewa Wayne Rooney na Shirikisho la Soka Ulaya-UEFA kufuatia kutolea nje katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya 2012 dhidi ya Montenegro mwezi uliopita. Msemaji wa FA amesema kuwa walipokea kwa maandishi sababu za kufungiwa kwa mchezaji huyo kutoka UEFA siku ya Jumanne mchana na walipewa muda wa kukata rufani kitu ambacho wamefanya. Kama ikibakia hivyo kufungiwa huko kwa mchezaji huyo kutamkosesha mechi tatu za mwanzo katika michuano hiyo ya Ulaya inayotarajiwa kuchezwa mwaka kesho.Mapema mchezaji huyo amesema hamlaumu mtu yoyote bali anajilaumu mwenyewe kwa kosa la kijinga alilofanya la kumkwatua kwa makusudi beki Montenegro Miodrag Dzudovic na akadai kuwa atamwelewa kocha Fabio Capello kama atamuacha katika kikosi kitachokwenda Poland kucheza michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment