PRINCE BOATENG ASTAAFU KUITUMIKIA BLACK STARS.
|
Kevin-Prince Boateng |
KIUNGO wa Kimataifa wa Ghana Kevin-Prince Boateng ametangaza kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya nchi hiyo Black Stars. Boateng ambaye ana miaka 24 amewahi kuichezea timu ya Taifa ya Ujerumani ya umri chini ya miaka 19 kabla hajabadilisha uraia na kuichezea Black Stars mwaka jana. Kiungo huyo wa AC Milan ambaye ameichezea Black Stars kwa miezi 18 amesema amefikia uamuzi huo kufuatia majeraha yanayomsumbua. Msemaji wa shirikisho la soka la nchi hiyo amesema wamepata barua kutoka kwa mchezaji huyo juu ya nia yake hiyo ya kustaafu kuichezea Ghana. Mchezaji huyo alifafanua kuwa ili aendelee vizuri kwa kutibu jeraha lake alipata ushauri kutoka kwa daktari wake na familia juu ya suala hilo na kuamua kujiondoa katika kikosi cha Black Stars katika kipindi hiki ambacho anafanya mazoezi maalumu kwa ajili kurudi katika kiwango chake ili aweze kuitumikia vyem klabu yake ya AC Milan.
No comments:
Post a Comment