Thursday, November 3, 2011

BLACK STARS KUJIPIMA NGUVU NA SENEGAL, IVORY COAST.

TIMU ya Taifa ya Ghana-Black Stars- inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya Senegal na Ivory Coast michezo ambayo itachezwa nchini Ufaransa. Senegal ndio watakaokuwa wa kwanza kuivaa Black Stars Novemba 11 mwaka huu kabla ya kupambana na Ivory Coast siku nne baadae, kiwanja kitakachotumika kwa ajili ya mechi hizo kitatangazwa hapo baadae. Black Stars haijawahi kucheza na Senegal katika kipindi cha miaka mitano toka wakutane mwaka 2006 katika michuano ya Mataifa ya Afrika ambapo Ghana ilishinda, huku mara ya mwisho timu hiyo kucheza na Ivory Coast ni mwaka jana jijini Cabinda, Angola katika michuano ya Mataifa ya Afrika ambapo Ghana walifungwa mabao 3-1.Timu zote tatu ndizo zinazopigiwa chapuo ya kufanya vizuri katika michuano ya Mataifa ya Afrika ambayo imeandaliwa kwa pamoja na Gabon na Equatorial Guinea inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 21, 2012 .

No comments:

Post a Comment