Thursday, November 10, 2011

BRAZIL YAILAZA GABON 2-0

Brazil imeifunga Gabon kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika jijini Libreville jana usiku. Lakini Brazil itabidi washukuru kumaliza mchezo huo bila ya kupata majeruhi kutokana na hali mbaya ya sehemu ya kuchezea iliyosababishwa na hali mbaya ya hewa na mchezo mbaya uliokuwa ukichezwa na wachezaji wa Gabon. Brazil walipata bao la kuongoza dakika 12 kupitia kwa mchezaji wake Alex Sandro baada ya kumalizia mpira uliokuwa umetemwa na golikipa wa Gabon Didier Ovono. Kiungo Hernanes aliipatia Brazil bao la pili dakika 10 kabla ya mapumziko kwa kichwa akimalizia krosi iliyopigwa na Jonas na kumpita Ovono kabla ya kumkuta kiungo huyo anayechezea klabu ya Lazio. Timu ya Brazil imekuja Afrika kwa mara ya kwanza toka walivyotolewa katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka jana ambapo wanatarajiwa kucheza mchezo mwingine na mabingwa wa Afrika Misri mchezo utakaofanyika jijini Doha, Qatar Jumatatu.

No comments:

Post a Comment