Thursday, November 10, 2011

BECKHAM, HENRY KUUNDA KIKOSI CHA WACHEZAJI NYOTA MAREKANI.

MCHEZAJI David Beckham ambaye mkataba wake na klabu ya Los Angeles Galax unakwisha mwishoni mwa msimu huu ametajwa kama mmoja wa wachezaji wanaocheza nafasi ya kiungo bora katika Ligi Kuu nchini Marekani-MLS. Beckham mwenye umi wa miaka 36 alitajwa na kuwa miongoni mwa wachezaji 11 bora kwa nafasi tofauti ambao huchaguliwa na wachezaji, viongozi wa vilabu na waandishi wa habari. Mchezaji huyo ambaye ameichezea Galax michezo 26 msimu huu ni kati ya wachezaji wa viungo watano walioitwa katika kikosi hicho cha wachezaji nyota wa ligi hiyo. Kiungo Landon Donovan ambaye anacheza timu moja na Beckham na ameteuliwa katika kikosi hicho pamoja na mshambuliaji Thierry Henry anayecheza katika klabu ya New York Red Bulls. Beckham anatarajia kucheza fainali yake ya kwanza ya Kombe la Ligi ya MLS toka ajiunge na Galax fainali ambayo itachezwa Novemba 20 dhidi ya Hoston.

No comments:

Post a Comment