Monday, November 7, 2011

CAF CHAMPIONS LEAGUE: ESPERANCE YALAZIMISHA SARE NYUMBANI KWA WYDAD.

Moja ya Hekaheka za mchezo baina ya Wydad na Esperance uliochezwa jana.
MSHINDI wa michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika anatarajiwa kupatikana mjini Tunis wiki ijayo baada ya Esperance ya Tunisia kuilazimisha sare ya bila kufungana nyumbani kwake Wydad Athletic ya Morocco katika mchezo wa kwanza wa fainali ya michuano hiyo uliochezwa jijini Casablanca Jumapili. Matokeo hayo ni mazuri kwa upande wa Esperance ambao walikuwa wakicheza ugenini huku mchezo wa pili ukichezwa nyumbani kwao, kwa upande wa Wydad matokeo hayo sio mazuri sana kwani walitakiwa washinde ili kujiweka katika nafasi nzuri. Wydad itabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kupata mabao baada ya kumiliki mpira karibu kipindi chote cha kwanza huku wachezaji wake Rami Yassine na Fabrice Ondama anayetokea Congo Brazaville kukosa mabao ya wazi. Esperance nao walizinduka kipindi cha pili ambapo nao wachezaji wake Mejdi Traoui na Khaled Mouelhi walikosa mabao ya wazi dakika za majeruhi. Mchezo wa pili ambao ndio utakaoamua mshindi wa michuano hiyo unatarajiwa kuchezwa Novemba 12 mwaka huu katika Uwanja wa Rades jijini Tunis, Tunisia.

No comments:

Post a Comment