Monday, November 7, 2011

CAPELLO AMUACHA ROONEY KATIKA KIKOSI CHAKE.

NAHODHA John Terry amejuimishwa katika kikosi cha Uingereza pamoja na uchunguzi unaoendelea juu yake kuhusu tuhuma za kutoa matamshi ya kibaguzi. Wayne Rooney yeye ameachwa katika kikosi kwa kuwa atakosa michuano ya Ulaya inayotarajiwa kufanyika mwaka 2012 baada ya kufungiwa mechi tatu na Shirikisho la Ulaya-UEFA. Wachezaji wengine ambao watakosa katika kikosi hicho ni pamoja na Rio Ferdinand, Micah Richard wa Manchester City na mshabuliaji wa Liverpool Andy Carroll. Kikosi kamili cha timu hiyo ambacho kitakwaana na Hispania pamoja na Sweden na timu wanazotoka katika mabano kitakuwa na Makipa: Joe Hart (Man City), Scott Carson (Bursaspor), David Stockdale (Ipswich); Mabeki: Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Man Utd), Gary Cahill (Bolton), John Terry (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Viungo: Leighton Baines (Everton), Phil Jagielka (Everton), Joleon Lescott (Man City), Kyle Walker (Tottenham); Frank Lampard (Chelsea), Jack Rodwell (Everton), Stewart Downing (Liverpool), Wakati washambuliaji watakuwa ni Gareth Barry (Man City), Adam Johnson (Man City), James Milner (Man City), Scott Parker (Tottenham), Theo Walcott (Arsenal); Darren Bent (Aston Villa), Daniel Sturridge (Chelsea), Gabriel Agbonlahor (Aston Villa), Bobby Zamora (Fulham), Danny Welbeck (Man Utd).

No comments:

Post a Comment