Monday, November 7, 2011

BASENA KUENDELEA KUINOA SIMBA.

Moses Basena
KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba mwishoni mwa wiki hii ilikutana kujadili mambo mbali kuhusiana na mwenendo wa klabu hiyo. Akizungumza Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa klabu hiyo Ezekiel Mwesigwa amesema kamati hiyo ili ilijadili mambo mbalimbali ikiwemo suala la usajili katika dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa. Amesema kwakuwa klabu hiyo ilisajili wachezaji 26 katika kipindi kilichopita katika usajili na kubakisha wachezaji wanne kamati hiyo waliafikiana kuziba hizo nafasi kwa kusajili wachezaji kutoka timu yao ya vijana wa umri chini ya miaka 20. Amesema lengo la kufanya hivyo ni ni kukuza vipaji vya vijana hao kama vilabu vingine vikubwa vinavyofanya katika nchi mbalimbali hususani Ulaya. 
Jerry Santo
Kamati hiyo pia ilijadili suala la mchezaji Jerry Santo ambaye amepata timu ya kucheza katika bara la Asia na kumpa baraka zote kwenda ambapo nafasi yake ya mchezaji wa kigeni itazibwa na mchezaji Derick Walulia kutoka Uganda. Mambo mengine ambayo yalijadiliwa na kamati hiyo ni pamoja na suala la mchezaji Kelvin Yondani na kusema kuwa wamepokea barua ingawa walikiri kuwa suala lake linaweza kuzungumzika lakini kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kuondoka. Pia Kamati hiyo ilitumia fursa hiyo kuomba radhi kwa mashabiki wake kwa kupoteza mchezo wake dhidi ya Yanga lakini waliwaomba mashabiki hao kuwa wavumilivu kwani timu yao bado ni imara ndio mpaka sasa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kamati hiyo pia imesema kwa kuzingatia matatizo yaliyompata kocha wake Moses Basena kwa kufiwa na mama yake mzazi wameamua kuhahirisha kuijadili ripoti yake ili kuungana nae katika kipindi hiki kigumu. Wakamalizia kuwa wataijadili ripoti pindi kocha huyo atapomaliza matatizo yake hivyo kocha huyo ataendelea kukinoa kikosi hicho cha Msimbazi.

No comments:

Post a Comment