Wednesday, November 16, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: KILIMANJARO STARS KUANZA KAMPENI YAKE DHIDI YA RWANDA.

Mabingwa watetezi wa michuano ya Afrika Mashariki na kati timu ya Tanzania Bara Kilimajaro Stars itaanza kampeni ya kutetea Ubingwa wake dhidi ya Rwanda katika michuano ya mwaka huu. Michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la vyama vya michezo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Cecafa inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Novemba 25 hadi Decemba 10 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa hii leo siku ya ufanguzi kutakuwa na michezo miwili ambapo timu ya Burundi itacheza dhidi yaSomalia wakati Zanzibar Heroes wakicheza dhidi ya Uganda. Kwa upande wake Rais wa Cecafa LEODGER TENGA amesema timu ya Eritrea imejitoa katika michuano hiyo hivyo nafasi kuchukuliwa na timu kutoka Namibia. Kuingia kwa Namibia kumefanya michuano ya mwaka huu kuwa na timu mbili ikiungana na Malawi ambayo ilishatangwazwa huko nyuma. Mashindano hayo yatafanyika katika kituo kimoja cha Dar es salaam kutokana na Mkoa wa Mwanza kushindwa kupata wadhamini wakuendesha mashindano Mkoani humo. Katika hatua nyingine TENGA ameipongeza timu ya taifa ya Tanzania taifa stars kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya kuwania kucheza fainali za kombe la Dunia mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment