Wednesday, November 16, 2011

UEFA 2012: HISPANIA, UHOLANZI KUONGOZA DRAW YA UEFA.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA wamethibitisha nchi za Hispania na Uholanzi ndio zitakuwa timu za juu pamoja na wenyeji Poland na Ukraine katika mchakato wa kupanga ratiba ya michuano ya Kombe la Ulaya 2012. Nchi za Ujerumani, Uingereza, Urusi na Italia zitakuwa zinafuatia katika mchakato huo unaotarajiwa kufanyika Desemba 2 mwaka huu jijini Kiev ambapo timu 16 zitagawanywa katika makundi. Nafasi za tatu zitakuwepo nchi za Croatia, Ugiriki, Ureno na Sweden wakati nafasi za nne zitakuwa nchi za Denmark, Ufaransa, Jamhuri ya Czech na Ireland. Katika taarifa yake UEFA imesema timu hizo zimepangwa kutokana na nafasi zao katika orodha ya timu bora duniani.

No comments:

Post a Comment