Saturday, November 19, 2011
CECAFA CHALLENGE CUP: UGANDA YATAJA KIKOSI CHAKE.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Uganda Bobby Williamson ameteua majina ya wachezaji 21 kwa ajili ya kuunda kikosi cha nchi hiyo kitakachopambana katika michuano Kombe la Challenge itakayoanza baadae mwaka huu jijini Dar es Salaam, Tanzania. Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza mazoezi rasmi Jumatatu Novemba 21 katika Uwanja wa Namboole jijini Kampala kabla ya kusafiri kuelekea Dar es Salaam baadae wiki ijayo. Akizungumzia suala hilo Ofisa Habari wa kikosi hicho alithibitisha uteuzi wa kikosi hicho ambacho amesema ni kikosi imara ambacho kitarejea na kombe hilo nyumbani. Kikosi hicho kinaundwa na makipa Adel Dhaira, Robert Odongkara na Ali Kimera, mabeki ni Simon Massa, Godfrey Walusimbi, Habibu Kavuma, Isaac Issinde, Andy Mwesigwa, Henry Kalungi. Wakati viungo watakuwa ni Mike Mutyaba, Sula Matovu, Moses Oloya, Vincent Kayizzi, Daniel Wagaluka, Tonny Mawejje, Mussa Mudde na Patrick Ochan huku washambuliaji wakiwa Brian Omony, Emmanuel Okwi, Mike Sserumaga na Robert Ssentongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment