Saturday, November 19, 2011

ETO'O, AYEW, GERVINHO, KEITA, YAYA KUGOMBEA TUZO ZA BBC.

SHIRIKA la Utangazaji nchini Uingereza-BBC limeteua majina ya wachezaji watano wa Afrika watakaogombania tuzo ya mwanasoka bora kutoka Afrika wa shirika hilo mwaka huu. Mwaka jana Asamoah Gyan ndio alishinda tuzo hiyo ambapo mwaka huu katika mchuano huo wapo Andre Ayew anayekipiga katika klabu ya Marseille, Samuel Eto’o anayekipiga klabu ya Anzhi ya Urusi, Seydou Keita anayechezea klabu ya Barcelona, na Gervinho anayecheza Arsenal pamoja na Yaya Toure anayecheza Manchester City. Mshindi wa tuzo hiyo atachaguliwa kwa njia ya kupigiwa kura na mashabiki kwa njia ya ujumbe mfupi na mtandao ambapo mwisho wa kuchagua itakuwa ni Desemba 9 na mshindi atatangazwa wiki moja baadae. Kwa miaka ya karibuni Ayew amekuwa mchezaji tegemeo kwa klabu yake pamoja na nchi ameweza kuisaidia nchi yake kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika huku akiiongoza klabu yake ya Marseille kombe la Ligi Kuu ya Ufaransa pamoja na Kombe la Chama cha Soka cha nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment