Saturday, November 19, 2011

CONFEDERETION CUP: AFRICAIN NA MAS KUPEPETANA LEO KATIKA FAINALI YA KWANZA.

KLABU Africain ya nchini Tunisia itaikaribisha timu ya MAS ya Morocco leo Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho mchezo ambao hautahudhuriwa na mashabiki uwanjani. Wanasiasa nchini Morocco wamelalamika jinsi baadhi ya mashabiki wa timu ya Wydad Casablanca walivyonyanyaswa jijini Tunis wakati wa mchezo wa fainali ya pili ya Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika dhidi ya Esperance. Pia kulikuwa matatizo kwa mashabiki hao ambao walikuja kuishangilia timu yao katika Uwanja wa Ndege wa Tunis wakati wakiwa wanarudi nyumbani. Hatahivyo suala la kucheza bila mashabiki katika mchezo wa leo haihusiani na suala hilo kwasababu timu ya Africain tayari walipewa adhabu kufungiwa kwa mashabiki wake kwa mechi mbili kufuatia vurugu zilizotokea katika mchezo wa makundi dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast. Klabu kongwe nchini Tunisia ambayo ina zaidi ya miaka 91 pia ilitozwa faini ya dola 100,000 na kuonywa kuwa endapo mashabiki wake wakirudia tabia za vurugu basi wataondolewa kabisa katika michuano hiyo na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF.

No comments:

Post a Comment