Saturday, November 19, 2011
BULGARIA WATOZWA FAINI KWA UBAGUZI.
SHIRIKISHO la Soka la Bulgaria-BFU limetozwa faini ya Euro 40,000 na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa ushangiliaji wa kibaguzi waliofanya mashabiki wa nchi hiyo katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya dhidi ya England uliofanyika mwezi Septemba. Katika taarifa yake waliyoituma kwa njia ya mtandao UEFA imesema mashabiki hao waliokuwa nyumbani walikuwa wakishangilia huku moja kwa moja wakiwatupia maneno ya kibaguzi wachezaji wa Uingereza katika mchezo wao huo uliofanyika jijini Sofia Septemba 2. Pamoja na juhudi za BFU kupinga masuala kibaguzi kumekuwa na matukio machache katika nchi ya Balkan katika miaka ya karibuni. Mashabiki wa klabu ya CSKA Sofia walikuwa wakipiga kelele za nyani kwa aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool Djibril Cisse wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwaka 2005. UEFA imewapa BFU siku tatu za kukata rufani kupinga adhabu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment