Saturday, November 19, 2011

MARADONA NAE AMSHUKIA BLATTER.

MCHEZAJI nguli wa soka wa Argentina Diego Maradona amedai hatua zichukuliwe dhidi ya Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu suala la ubaguzi kwenye mchezo mapema wiki hii. Blatter alitoa kauli iliyoleta utata miongozi mwa wadau wengi wa mchezo huo akidai suala la ubaguzi baina ya wachezaji halipo na kama likitokea basi linaweza kumalizwa na wachezaji wenyewe kwa kushikana mikono baada ya mchezo.
Maradona akihojiwa juu ya suala hilo wakati na mkutano na waandishi wa habari huko Falme za Kiarabu-UAE amesema bosi huyo wa FIFA ameshafanya makosa mengi kabla mengine yakitokana na maamuzi yake na mengine kauli zake hivyo hiyo sio mara yake ya kwanza. Maradona aliongeza kusema kuwa ubaguzi haukubaliki na Blatter na FIFA huwa wanachukua hatua haraka kwasababu matokeo yake huwa sio mazuri kwa mchezo hivyo vitendo vinatakiwa kupingwa vikali lakini akahoji kwanini hatua hazichuliwi dhidi ya bosi huyo. Kwasasa Maradona ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Argentika katika fainali za Kombe la Dunia lililofanyika Afrika Kusini mwaka 2010 anakinoa kikosi cha timu ya Al Wasl ya huko Uarabuni.

No comments:

Post a Comment