Monday, November 14, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: WAAMUZI 19 WAINGIA KATIKA USAILI.

BARAZA la Soka kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati-CECAFA limeteua waamuzi 19 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Challenge inayotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 25 mpaka Desemba 10 mwaka huu. Kenya ndio imetoa waamuzi wengi zaidi ktika uteuzi huo ambao ni Davies sagero, Brasan Mamati na Davies Omweno wengine ni Denis Batte (Uganda), Bamlak Tessema(Ethiopia), Wish Yabarow (Somalia) na Eric Gasinzigwa (Burundi). Waamuzi wasaidizi watakuwa ni pamoja na Hassan Yacin Egueh (Djibouti), Idam Mohamed Hamid (Sudan), Yohanes Girmai (Eritrea) na Mark Sonko (Uganda). Waamuzi hao wanatarajiwa kupewa semina na majaribio kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya michuano hiyo itayochezwa katika miji miwili Dar es Salaam na Mwanza ambapo mwishoni mwa semina hiyo waamuzi wote watafanyiwa vipimo vya afya na watakaofaulu ndio watakaoteuliwa kuwa waamuzi wa michuano hiyo. Wenyeji Kilimanjaro Stars ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo walishinda mwaka jana baada ya kuifunga Ivory Coast kwa 1-0 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment