Thursday, November 24, 2011

CECAFA CHALLENGE CUP: ZANZIBAR KUANZA NA UGANDA LEO.

MICHUANO ya kombe la Challenge inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika michezo ya leo ya kundi B Zanzibar itakuwa kibaruani kupambana na Uganda mchezo ambao utachezwa jioni wakati katika mchezo wa kwanza Burundi itapepetana na Somalia.
Mara ya mwisho Uganda na Zanzibar zilikutana katika robo fainali ya michuano hiyo mwaka jana na Uganda ilifanikiwa kuitoa Zanzibar kwa penalti 5-3, baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida. Akihojiwa kocha wa Zanzibar Hemed Morocco amesema mchezo huo utakuwa ni mgumu kwakuwa Uganda ni timu nzuri lakini akaahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha timu yake inaondoka na ushindi katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment