Thursday, November 24, 2011

BESIKTAS YAFUNGIWA MECHI MOJA.

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Uturuki-PFDK limeifungia klabu ya Besiktas kucheza mchezo wao mmoja wa nyumbani bila mashabiki kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa mchezo wao na Galatasaray. Klabu hiyo pia imepigwa faini ya euro 94,000 kwa ajili la tukio hilo lililotokea wiki iliyopita katika uwanja wake uitwao Inonu. Mchezaji wa Galatasayar Emmanuel Eboue ndiye alikuwa mhanga katika tukio hilo ambapo mashabiki hao wenye hasira walimpiga na vitu mbalimbali ikiwemo chupa za maji na viberiti vya gesi wakati wa mchezo huo. Wakati huohuo mchezaji wa kimataifa wa Brazil Felipe Melo amefungiwa kucheza mchezo mmoja kwa kosa la kugombana na mashabiki hao, Besiktas inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu nchini humo wakati Galatasayar wao wanashika nafasi ya tatu.

No comments:

Post a Comment