Thursday, November 24, 2011

BRAZIL YAZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UBAGUZI.

Waandaaji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 Brazil wamezindua kampeni ya kupinga suala la ubaguzi wa rangi michezoni Alhamisi hii. Shirikisho la Soka la Brazil-CBF wametaja mzunguko wa mechi za ligi kuu ya nchi hiyo zinazochezwa wiki hii kuwa ni mzunguko wa kupinga ubaguzi. Katika taarifa yake CBF wamesema suala la ubaguzi haliwezi kutatuliwa kwa kushikana mikono wakipinga na kauli ya kushtusha aliyoitoa Rais wa FIFA Sepp Blatter aliyesema masuala ya ubaguzi michezoni yanaweza kumalizwa na wachezaji wenyewe kwa kushikana mikono baada ya mchezo. Kauli ilileta utata na kukemewa na wadau wengi wa mchezo huo mpaka ikamlazimu Blatter kuomba radhi kwa kauli yake hiyo.

No comments:

Post a Comment