Thursday, November 24, 2011

MARADONA ASHUKURU WALIOMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA KUFIWA NA MAMA YAKE.

Mchezaji nguli wa soka wa Argentina Diego Maradona ametoa shukrani kwa wote waliomtumia ujumbe mfupi wa kumpa pole kufuatia kifo cha mama yake Dalma Franco. Mchezaji huyo ambaye alikiongoza kikosi Argentina kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka 1986 amesema kuwa anawashukuru wote pamoja na wale waliokaa kimya dakika moja kutoa heshima zao kwa mama huyo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini Argentina. Maradona ambaye ana miaka 51 amesema pia ameguswa na ujumbe aliotumiwa na Rais wan chi hiyo Cristina Kirchner pamoja na majirani wa mji Villa Fiorito ambao ndio nyumbani kwa mchezaji huyo. Mchezaji huyo ambaye anaifundisha klabu ya Al-Wasl ya Falme za Kiarabu aliondoka huko Jumapili iliyopita kuja kumuuguza mama yake lakini akiwa njiani alijulishwa kuwa mama yake huyo alikuwa amefariki dunia. Mojawapo ya watu wengine maarufu waliotuma slamu zao rambirambi kwa mchezaji huyo ni pamoja na muigizaji Ricardo Darin, bingwa wa zamani wa michuano ya tenisi ya wazi ya Marekani mwaka 2009 Juan Martin Del Porto, mcheza soka Martin Palermo pamoja na nyota wa Barcelona Lionel Messi.

No comments:

Post a Comment