Thursday, November 24, 2011

MILAN YAANZA MAZUNGUMZO NA TEVEZ.

KLABU ya AC Milan imeanza mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez kuhusu uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo katika kipindi cha dirisha dogo la usajili. Tevez amekuwa katika misukosuko na City toka mwanzoni mwa msimu ambapo alitaka kuondoka na wiki chache zilizopita alipigwa faini na klabu hiyo kwa kukataa kupasha misuli moto wakati wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich mwezi uliopita. Mchezaji huyo ameichezea klabu hiyo mara chache msimu huu akiwa na Edin Dzeko, Mario Balotelli, Sergio Aguero na David Silva wakiunda safu ya ushambuliaji. Milan wako sokoni wakitafuta mshambuliaji mbadala baada ya Antonio Cassano kufanyiwa upasuaji wa moyo baada ya kuugua ghafla wakati wa mchezo dhidi Roma ambao walishinda mabao 3-2, mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja msimu wote huu.

No comments:

Post a Comment