Kikosi kamili cha timu hiyo na timu wanazotoka katika mabano kitakuwa na makipa: Boubacar Barry (Lokeren), Gnanhouan Gerard (Avranches), Daniel Yeboah (Asec), mabeki: Benjamin Angoua (Valenciennes), Souleiman Bamba (Leicester), Emmanuel Eboue (Galatasary), Igor Lolo (Kuban), Siaka Tiene (PSG), Kolo Toure (Manchester City), Didier Zokora(Trabzonspor). Wakati viungo watakuwa: Jean-Jacques Gosso (Orduspor), Max Gradel (Saint-Etienne), Coulibaly Kafoumba (Nice), Didier Ya Konan (Hanover), Yaya Toure (Manchester City) na washambuliaji: Wilfried Bony (Vitesse), Seydou Doumbia (CSKA Moscow), Gervinho (Arsenal), Salomon Kalou (Chelsea)
Tuesday, November 8, 2011
DROGBA NJE KIKOSI CHA IVORY COAST.
KOCHA wa Ivory Coast Francois Zahoui ametangaza kikosi kwa ajili ya mchezo dhidi ya South Afrika wa Kombe la Nelson Mandela bila ya nahodha wake Didier Drogba mchezo utakaochezwa Novemba 12 mwaka huu. Drogba amepumzishwa kwenye mchezo huo kufuatia upasuaji wa mkono aliofanyiwa hivi karibuni kuondoa vyuma alivyowekewa mkononi kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwaka jana baada ya kuvunjika mkono huo. Kocha huyo ameita kikosi cha wachezaji 19 kikiwa na nyota wote wanaocheza soka Ulaya wakiwemo Gervinho anayekipiga Arsenal, Kolo na Yaya Toure wanaocheza Manchester City na winga wa Chelsea Salomon Kalou. Mbali ya hao pia yumo beki wa kulia Guy Demel anayekipiga West Ham wakati Cheick Tiote anayekipiga Newcastle na kiungo mchezeshaji wa timu hiyo anayekipiga Al Saad wenyewe hawakujumuishwa katika kikosi hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment